Parliament of Tanzania

Bunge la Bajeti laanza Jijini Dodoma

Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge umeanza Jumanne tarehe 2 Aprili 2019 na unatarajiwa kumalizika tarehe 28 Juni 2019 Mjini Dodoma. Mkutano huu utakuwa ni mahsusi kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa Bajeti za Wizara kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

1.0 MASWALI

Katika Mkutano huu wa Kumi na Tano, wastani wa maswali 515 ya Kawaida yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa na Serikali Bungeni. Aidha, wastani wa Maswali 88 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yanatarajiwa kuulizwa kwa siku za Alhamisi.

2.0 KUJADILI HOTUBA YA HALI YA UCHUMI NA BAJETI YA SERIKALI

Bunge litajadili Hotuba ya Hali ya Uchumi wa Taifa na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 itakayowasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango.

3.0 MISWADA YA SERIKALI

Bunge pia linatarajia kujadili na kupitisha Miswada Miwili (2) ya Sheria ambayo itasomwa kwa hatua zake zote. Miswada hiyo ni:-

· Muswada wa Sheria ya Fedha za Matumizi wa mwaka 2019 (The Appropriation Bill, 2019)

· Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019.

Ratiba yote ya Mkutano huu

Hon. Dr. Tulia Ackson

Speaker

Legislative Role

Profile

Ask the Speaker / Comments

Ms. Nenelwa J. Mwihambi

Clerk of the National Assembly

Legislative Role

Profile

Ask the Clerk / Comments

View All MP's