United Republic of Tanzania
Parliament of Tanzania
All Contributions |
---|
Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 – Wizara ya Maliasili na UtaliiMHE. HAROON M. PIRMOHAMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Taifa Ruaha na vijiji vinavyopatikana na vilivyomo ndani ya Hifadhi ya Ruaha umedumu takribani miaka tisa sasa tangu mwaka 2008. Hivi karibuni Serikali ilitoa maelekezo ya kushughulikia mgogoro wa mpaka huo ili uweze kuisha na wananchi waendelee na shughuli zao za maendeleo. |