" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa barabara nyingi zinazungumziwa urefu hata hii barabara inayolalamikiwa hapa.
Lakini hazijazungumziwa barabara upana wake na tunavyofahamu ni kwamba barabara ndefu kama inayotoka Morogoro au ya Bagamoyo au barabara nyingine hizi. Kama Wakandarasi watakuwa wamepunguza inchi moja ama mbili katika upana wa barabara zile basi inakuwa ni hasara kubwa sana katika nchi?
Je, Naibu Waziri anaweza kuniambia upana wa barabara hizi hasa barabara ya Morogoro kuja Dar es Salaam au barabara ya Morogoro kuja Dodoma zina upana gani na je, ananiruhusu mimi kutembea na futi na kupima wakati wowote unaofaa? Ahsante.
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 338
SESSION # 4
Answer From Hon.Sitta, Samuel John
INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT
SPIKA:
Nasikitika swali hilo liko nje ya swali la msingi. Kwa sababu swali la msingi limehusu barabara ya Dar es Salaam.