" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kuniona na nimshukuru sana Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani kwa majibu yake mazuri. Nina swali moja la nyongeza, suala la ajali halisababishwi na magari peke yake lakini pia suala ajali ambalo pia limemwondosha mwenzetu juzi limesababishwa pia na udhaifu wa barabara ambapo wakati mwingine madereva wanashindwa kuhimili gari kutokana na hali ya barabara ilivyo.
Kwa mfano pale Kilosa, Berega, ambapo sasa ilishatokea ajali zaidi ya sita kutokana na kipande kidogo tu cha barabara ambacho kinaudhaifu wa utengenezaji. Je, Mheshimiwa Waziri anaiambia nini Bunge hili Tukufu kuhusu marekebisho ya kipande kile ili Watanzania wasipoteze maisha yao katika barabara ile?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 105
SESSION # 15
Answer From Hon.Kagasheki, Ambassador Hamis Suedi
HOME AFFAIRS
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:
Mheshimiwa Spika, kwa kweli tunao mgawanyo wa shughuli katika Serikali upande wa Wizara yangu kama anavyofahamu tuko upande katika kui-force zile sheria tulizonazo katika barabara. Upande wa kutengeneza barabara na kusema barabara zimekaaje huo ni upande wa wenzetu wa Miundombinu. Lakini kwa kuwa umeuliza hili suala tutalifikisha kwa wenzetu wa Miundombinu na kuhakikisha kwamba unapata jibu sahihi kwa sababu siwezi nikakupa mimi jibu sahihi kwamba barabara itatengenezwa au kipande hicho kitarekebishwa namna gani.