|
|
| Home »Supplementary Question |
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Kevela, Stanley Jilaoneka Yono[CCM]
Njombe Magharibi Constituency |
|
|
|
|
|
|
| 8 |
101 |
INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT |
Transport/Road |
28 June 2007 |
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa barabara ya Njombe ¿ Lupembe inalingana kabisa na ile barabara ya Njombe ¿ Makete, yaani kupitia Kata ya Igosi na Kipengele; na kwa kuwa hii barabara ya Njombe ¿ Makete mara nyingi inapojengwa inawekwa kifusi cha udongo, siyo cha kokoro na hivyo kusababisha kwamba sasa hivi haipitiki, ina mashimo marefu sana na kuleta kero kubwa kwa wananchi wa Igosi, Kipengele, Makete na Njombe kwa ujumla. Je, ni lini Serikali itaweka kifusi cha kokoto kuliko ilivyo sasa hivi kuweka kifusi cha udongo mpaka kusababisha usumbufu mkubwa sana katika Jimbo letu la Njombe hasa Wilaya ya Njombe na Mkoa wa Iringa kwa ujumla?
|
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 101
SESSION # 8 |
 |
Answer From Hon.Mahanga, Dr. Milton Makongoro
INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT |
|
NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU :
Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hiyo ya Njombe ¿ Makete imekuwa ikitengenezwa kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge. Lakini, kutokana na ufinyu wa Bajeti, matengenezo hayajawa makubwa kama ambavyo angependa au ambavyo na sisi tungependa. Hata hivyo, katika mwaka huu ujao wa fedha, bado fedha zimewekwa kwa ajili ya kuendelea kutengeneza barabara hiyo ya Njombe ¿ Makete ambayo hata mimi niliikagua na nikaona hali hiyo. Tuombe kwamba fedha zikiwa zinatosheleza, basi itatengenezwa kwa kiwango ambacho kitaridhisha ili barabara hiyo ipitike mwaka mzima. |
|
Records 1 to 1 of 27 |
|
|
|
|
|