|
|
| Home »Supplementary Question |
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Karamagi, Nazir Mustafa[CCM]
Bukoba Vijijini Constituency |
|
|
|
|
|
|
| 20 |
44 |
INDUSTRIES, TRADE AND MARKETING |
Business |
14 June 2010 |
Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
(i) Kigoma ni Mkoa ambao uko pembezoni kama Mkoa wa Kagera; kwa sababu sasa hivi tunazungumzia masuala ya kibiashara ya kimataifa; Wizara ina mpango gani wa kutenga maeneo katika Mikoa ya Kigoma na Kagera ambayo inaweza kuwa kama Bonded Warehouse ama EPZ au SEZ kusudi nchi hizi ziweze kupata masoko ya sehemu za Magharibi kama DRC, Rwanda na Uganda?
(ii) Kama nilivyosema Mkoa wa Kigoma ni kama Mkoa wa Kagera; tuna maeneo ambayo yako mpakani na nchi hizi kama Mtukula kwa upande wa Nkenge kwa Mheshimiwa Kamala na Kata ya Rubafu katika Jimbo la Bukoba Vijijini ambapo sasa hivi kunajengwa Kivuko cha kuunganisha Tanzania na Uganda: Je, kuna mpango gani wa kufikisha umeme kwenye maeneo haya kusudi tuweze kunufaika na biashara ambayo inapatikana nchi za jirani?
|
| ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 44
SESSION # 20 |
 |
Answer From Hon.Chami, Dr. Cyril August
INDUSTRIES, TRADE AND MARKETING |
|
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO:
Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, changamoto ambazo Mkoa wa Kigoma unazikabili ni sawa na zile za Mkoa wa Kagera na kwa hiyo, umuhimu ambao tunauweka kwa Mkoa wa Kigoma vilevile tunauweka kwa Mkoa wa Kagera. Kuhusu maeneo maalum ambayo anayazungumzia hapa ya SEZ na EPZ, napenda nimhakikishie kwamba, Wizara yetu kwa kupitia Mamlaka ya Kuhimiza Mauzo Nje, tumetenga maeneo 14 katika nchi nzima ya Tanzania na eneo mojawapo lipo katika Mkoa wa Kagera.
Endapo atahitaji takwimu zaidi tutampatia ili aweze kufahamu eneo lipi ambalo tumelitenga, changamoto tuliyonayo sasa hivi ni kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza maeneo hayo yote katika Nchi ya Tanzania lakini la Kagera lipo. Kuhusu la umeme, napenda nimwambie Mheshimiwa Karamagi kwamba, tunaona umuhimu wa kuwa na umeme katika maeneo hayo na Serikali imesikia, tutaliwasilisha katika Wizara husika kuhakikisha kwamba, tunapofungua hicho kivuko basi kunakuwa na umeme ili mambo yote yaende sawa sawa kwa pande zote.
|
|
Records 1 to 1 of 1 |
|
|
|
|
|