" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
A by-election occurs when a seat in the National Assembly becomes vacant during the lifetime of a Parliament (i.e. between general elections).
What is the Cabinet?
The Ministers of the Government are known as the Cabinet. The President appoints ministers, including the deputy ministers that form the Cabinet, who often work in a government department, and run and develop public services and policies.
Nashukuru sana Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kunipa nafasi ili niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa pesa hizi zinazotolewa kama milioni 700 ambazo zimetolewa Wilayani Geita huwa zinachelewa sana kutolewa hasa tunapopitisha kwenye bajeti na kupelekea zinapofika mawilayani unakuta kwamba zinakuja kwenye mwezi wa kwanza kwenye mwaka unaofuata. Hivyo kusababisha pesa nyingi katika Halmashauri karibu zote huwa zinarudi za matengenezo ya barabara. Je, Serikali inasemaje ili kuweza kuwahisha tunapopitisha hapa tu basi pesa zinapelekwa katika wilaya zetu. Serikali inasemaje katika suala hili ?
ANSWERS TO SUPPLEMENTARY QUESTION # 104
SESSION # 12
Answer From Hon.Mwanri, Aggrey Deaisile Joshua
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT
NAIBU WAZIRI OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA:
Mheshimiwa Naibu Spika,
Ndiyo nitaeleza kwa kifupi. Tutakachofanya sisi kama Serikali na maelekezo yameshatolewa tayari na wala sio hela hizi tu zinazozungumzwa za barabara. Hata zile za Qwick Wins hata za MMES na MMEM zote mpango wa Serikali ni kuhakikisha kwamba hela hizi zinakwenda haraka iwezekanavyo ili ziweze kufanya kazi hizi za maendeleo kama ilivyotarajiwa.