ASK THE SPEAKER
GIF

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER
QUOTES FROM THE SPEAKER
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
5th March 2009 - Dar es Salaam.
INVITATION FOR TENDERS
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more
RESOURCES LINKS

Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project

WEBMAIL LOGIN


NEWSLETTER
Subscribe to our e-newsletter and be the first to know about new activities, events and resources.
Your email
GLOSSARY
Code of Conduct
helps MPs understand their responsibilities to Parliament and the public. In addition to guidance, the Code also requires all Members to declare outside interest, like paid work or gifts
Constituent
is the name given to every person who lives within or is eligible to vote in a constituency. The Tanzania is divided into 232 different regions – called constituencies – where the public elect candidates to be their MP.
Read more
VISITORS TO THIS SITE
There have been 30606876 visitors to this websiteThere have been 30606876 visitors to this websiteThere have been 30606876 visitors to this websiteThere have been 30606876 visitors to this websiteThere have been 30606876 visitors to this websiteThere have been 30606876 visitors to this websiteThere have been 30606876 visitors to this websiteThere have been 30606876 visitors to this website
User online : 12
Home »Pm questions & answers
Pm questions & answers
  email E-mail this to a friend email Printable version
Date Session Sitting
29 October 2009 17 3
Hon Mohamed, Hamad Rashid[CUF]
Mheshimiwa Spika ahsante sana, tarehe 9 Septemba, 2009, Tume ya Uchaguzi Taifa ilichoma moto shahada za Wapiga Kura pale Bohari Kuu Dar es Salaam.

Je, Waziri Mkuu angetueleza ni utaratibu gani Tume iliutumia ya kukusanya kadi hizo na kufikia idadi ya kuweza kuchomwa?
Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Spika, nilitaka kusema akichelewa mtu kama Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, usimruhusu mwache hivyo hivyo.

Itakuwa vigumu kujibu swali la Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed kwa sababu sina maelezo fasaha ambayo ningeweza nikayatoa na ni jambo kubwa kwa hivyo nafikiri ninachoweza kuahidi tu ni kwamba basi ebu niachie nilitazame niwasiliane na wenzangu tuone kilichotokea hasa ni nini na kama unavyosema sasa tunafanyaje, maana nikiamua tu kukupa blabla hapa nadhani haitasaidia sana.
Hon Mohamed, Hamad Rashid[CUF]
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwa kuwa jambo lenyewe kama unavyosema Mheshimiwa Waziri Mkuu ni kubwa na nakushukuru sana kwa hekima yako na busara yako uliyoitumia katika kulijibu hili swali la kwanza.
Je, huoni kwamba ni vyema kuwa jambo lenyewe ni kubwa tukaunda katume kidogo tukachunguza undani wa jambo lenyewe hasa kwa kutilia maanani kwamba Tume ya Uchaguzi ya Taifa imeshutumiwa sana kwa kutokuwa na uadilifu, ili kuisafisha hii Tume kwanini tusiunde katume kidogo kulichunguza jambo lenyewe ili tupate uhakika wake?
Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Spika, bado nitasimamia palepale kwamba naheshimu sana mawazo yake lakini mimi nafikiri busara nzuri ni kunipa nafasi nilifanyie kazi.
Hon Chegeni, Dr. Raphael Masunga[CCM]
Mheshimiwa Spika ahsante, Mheshimiwa Waziri Mkuu hivi karibuni kumetokea mtafaruku wa kimashindano ya kibiashara kati ya Tanzania Breweries na Serengeti Breweries, kitu ambacho kinapelekea baadhi ya maeneo kuleta uvunjifu wa amani. Mashindano haya ya kibiashara yanaweza kuwa na tija lakini kuwa na hasara kubwa sana kwa nchi na hasa kiuchumi. Je, Mheshimiwa Waziri Mkuu suala hili unalifahamu na kama unalifahamu ni nini mkakati wa Serikali wa kuzuia ushindani usiokuwa na tija kwa faida ya nchi?
Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Spika, naomba nijaribu tu kueleza kidogo juu ya jambo hili kwa sababu na lenyewe sina undani wake kwa sasa. Lakini anapozungumza kwamba inaweza kupelekea uvunjifu wa amani sasa unakuwa umeelekea katika jambo ambalo linataka nalo lifanyiwe kazi, ni kwa maana gani hasa tunalisema hivyo lakini mimi nadhani, kubwa kwanza ni kukubali tu kwamba tuko katika mfumo wa soko ambalo ni huru, makampuni mbalimbali ya binafsi yanaendesha shughuli zake kwa mujibu wa taratibu na Sheria zilizowekwa.

Ni kweli kumekuwa na hali ya mvutano na malumbano kati ya Serengeti Breweries pamoja na East Africa Breweries na Tanzania Breweries kwa ujumla; na nilipata mimi nafasi ya kukutana na Mzee Mark Bomani pamoja na mmoja wa wana hisa wakubwa sana katika ile kampuni na nikazungumza nao kwa kirefu sana na nilichowaasa mimi ni kwamba, kwangu mimi kwa kadri ninavyofahamu kama Mtanzania ni vyema bado Serengeti Breweries katika kulinda heshima na vilevile kutoa ile kiburi cha Mtanzania naye anapofanya vizuri kuendelea kuonekana kwamba anafanya vizuri badala ya kuingia katika mvuto wa kitu kinachofanya vizuri kwenda tena kukiuza kwa mtu mwingine ambaye mimi naamini mwisho wa yote itakuwa ni kuiua kabisa hiyo kampuni na tutajikuta hatuna faida tutakayoipata.
Mheshimiwa Spika, jambo hili alilielewa na mimi napenda niamini kwamba sidhani kama watakuwa wamebadilika sana kwa sababu tangu wakati ule sina taarifa za kutosha lakini naweza nikamwahidi Ndugu Chegeni kwamba kwa masilahi ya nchi yetu pengine ni jambo ambalo tunaweza tukajaribu kulifuatilia tena tuone limefikia wapi na tunaweza kushauri nini mbele ya safari.

  Records 1 to 3 of 12
 
Next Last
WHO IS WHO
Hon.Lotto, Sameer Ismail
bunge
Morogoro -Kusini -Mashariki Constituency
Questions(0)
Supplementary Questions(2)
Contributions(12)
More Members »


POLIS DATABASE
polis
BUDGET 2010/11
Estimate of Public Expenditure Development votes and supply vote
SEARCH FOR MP
Region
Constituent
 
VIDEO /AUDIO CLIP
More Videos
PHOTO GALLERY
Police parading(Saluting)the President Jakaya Kikwete when arrived to the Bunge Complex in Dodoma on 21.8.2008.
More photos
CALENDAR OF EVENTS
 <<  < Sep 2010 >   >>
SMTWThFS
1234
56789
10
11
12131415161718
19202122232425
2627282930

More events

Copyright © 2003-2008 Tanzania Parliament. All rights reserved.
Designed and published by DataVision International (T) Ltd
Terms of Use | Disclaimer