ASK THE SPEAKER
GIF

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER
QUOTES FROM THE SPEAKER
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
5th March 2009 - Dar es Salaam.
INVITATION FOR TENDERS
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more
RESOURCES LINKS

Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project

WEBMAIL LOGIN


NEWSLETTER
Subscribe to our e-newsletter and be the first to know about new activities, events and resources.
Your email
GLOSSARY
What's a Whip?
Whips are MPs appointed by each party to help organise their party’s contribution to parliamentary business. One of their responsibilities is making sure the maximum number of their party members vote, and vote the way their party wants. Whip is the key person in parliamentary system. The duties of bringing together member of the same political party and other parties are the prerogative of Whips. Standing Orders recoginse the Office of Chief Whips for both Ruling and Opposition parties, as well as the Assistant Whips for both parties.
Who is the Prime Minister?
When the results of a General Election are known the President appoints the Prime Minister who becomes the leader of the Government in the Parliament. The Leader of Government Business in the House is the Prime Minister who is assisted by all Ministers concerned primarily for organising the Business and for providing reasonable facilities for the House to debates matters about which it is concerned. The current Prime Minister is the Hon. Mizengo Kayanza Pinda MP.
Read more
VISITORS TO THIS SITE
There have been 30502591 visitors to this websiteThere have been 30502591 visitors to this websiteThere have been 30502591 visitors to this websiteThere have been 30502591 visitors to this websiteThere have been 30502591 visitors to this websiteThere have been 30502591 visitors to this websiteThere have been 30502591 visitors to this websiteThere have been 30502591 visitors to this website
User online : 15
Home »Pm questions & answers
Pm questions & answers
  email E-mail this to a friend email Printable version
Date Session Sitting
24 June 2010 20 15
Hon Zambi, Godfrey Weston[CCM]
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kumwuliza swali Mheshimiwa Waziri Mkuu swali.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, hivi karibuni na zaidi siku ya jana tarehe 23 Juni, 2010 nimepata simu nyingi sana kutoka Mbozi. Wafanyabiashara wa maduka ya madawa wamelalamika sana kwamba wananyanyaswa kwa sababu wameambiwa sasa wafunge maduka yao kama yamekaribiana na sharti linalotolewa ni kwamba kuwe na umbali wa mita 300 kutoka duka moja hadi jingine. Sasa mimi nashangaa ni sheria gani hii ya ubaguzi ambayo inamlazimisha mfanyabishara wa duka la dawa asifungue biashara pale anapotaka ila afungue pale tu ambapo mamlaka inayostahili inataka. Nataka ufafanuzi wa Serikali kwa sababu hii imeonyesha kama kuna ubaguzi mkubwa sana.

Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabla sijamjibu ndugu yangu Godfrey W. Zambi, niwashukuru sana Wabunge, muendelee na kasi hii mpungue zaidi maana mnanipunguzia pressure mimi. Lakini hiyo ni ishara vilevile watu wa Rukwa wakati mwingine tukifanya vitu vyetu mambo si mabaya sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa bahati mbaya ndiyo kwanza napata taarifa hii na bahati mbaya hapa katikati sikusaidiwa sana kwenye vyombo vya habari ili niweze kujua ni nini kinaendelea, mambo yalikuwa mengi!

Lakini kwa upande mmoja nataka niamini kwamba jambo hilo litakuwa limetokana pengine na taratibu zilizopo kuhusiana na masuala haya ya maduka ya dawa za binadamu, ni kama ilivyo tu kwa vituo vya mafuta, vituo vya mafuta navyo vina utaratibu kama huo ili kuweza kufanya pengine shughuli zifanyike vizuri zaidi.

Lakini linalonipa tatizo ni kwa kuwa hawa watu tayari walikwishaweka maduka hayo, kwa hiyo, kama kweli Serikali tungetaka kufanya kazi yetu iwe makini wakati wa kutoa leseni ndiyo tulitakiwa tufanye vilevile zoezi la kuhakiki na kuona duka hili liko umbali gani kutoka duka lingine badala ya kungoja watu wameshaweka miundombinu tayari wanauza dawa baadaye tena mnakurupuka mnaanza kupambana na watu katika mazingira ambayo kusema kweli hayana tija sana.

Lakini Mheshimiwa Zambi nataka nikuahidi kwa sababu Waziri wa Afya yuko hapa tutalishughulikia jambo hili mapema na mimi nataka niwasihi sana ambao waliamua kufanya hivi wasubiri kwanza kidogo tuelewane nini hasa kimetokea kwa sababu ni mara ya kwanza tunasikia utaratibu kama huo unajitokeza.
Hon Zambi, Godfrey Weston[CCM]
Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu yake.

Lakini kwa sababu pale Mbozi pia pamekuwa na malalamiko hasa miji ya Vwawa na Mloo na Mkoa wa Mbeya lilitokea hili kwamba wafanyabiashara wa kawaida ndiyo wanaokumbwa zaidi na msukosuko huu kuliko wafanyabiashara wenyewe ambao wako kwenye Sekta ya Afya kwa maana ya Madaktari na wengine wanaofanana nao.

Je, sasa utaagiza Mamlaka ya Mkoa wa Mbeya na Wilaya ya Mbozi kwa ujumla ili wahakikishe kwamba taratibu zinazingatiwa na ubaguzi hautokei katika suala hili?
Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Naibu Spika, nadhani kama nilivyosema Mheshimiwa Godfrey Zambi tupe nafasi tulifanyie kazi jambo hili, hata hilo unalolisema inawezekana lipo kwa sababu hatuwezi kukataa haraka haraka kabla hatujafanya uchunguzi.

Tukishabaini mambo yalivyo nadhani tutatoa maelekezo haraka sana ili kuweza kurekebisha kasoro ambayo inaweza kuwa imejitokeza na hiyo itawahusu hata Wataalamu wale wa eneo hili la Madaktari na watu wengine ambao wanahusika na jambo hili.
Hon Ligallama, Castor Raphael[CCM]
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi kumwuliza Waziri Mkuu swali moja.

Mheshimiwa Waziri Mkuu, Wilaya ya Kilombero ina eneo takribani la kilomita za mraba 15,000, lina watu wasiopungua 363,000, kutoka mwanzo wa Wilaya mpaka mwisho ni kilomita 300, lina kata 23, lina tarafa 5, vijiji 90, vitongoji 366.

Sasa ni kigezo kipi hasa tunachokosa sisi wana Kilombero kugawa hili jimbo au Wilaya hasa ukichukulia kwamba hii idadi ya watu 363,333 ni kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.

Lakini kati ya 2002 na leo hii 2010 kuna watu wengi wameingia katika Wilaya ile takribani wanafika karibu 100,000 nzima kwa hiyo, watu kwa idadi tunaweza tukafikia lake nne na kitu.

Sasa jimbo hili hasa na sehemu uliyofika Mheshimiwa Waziri Mkuu pale kwenye Bonde la Kihansi ni nusu tu.

Ni kigezo kipi kilichofanywa katika kugawa Wilaya na Wilaya hii isigawanywe?
Answer From Prime Minister
Mheshimiwa Naibu Spika, anachokisema Mheshimiwa Castor R. Ligallama, kuhusiana na eneo au Jimbo lake ni kweli, ni Jimbo kubwa bahati nzuri mara ya mwisho nilitembelea kule niliona hali halisi.

Lakini kwa upande mmoja Mheshimiwa Mbunge, Serikali katika suala la ugawaji wa maeneo mapya kinachotokea kwanza ni maombi kutoka kwa wahusika wenyewe wanaoona kwamba iko haja ya kugawa eneo katika maeneo ama Jimbo ama Wilaya.

Sina hakika kwa upande wa Kilombero kama maombi haya yaliwasilishwa au hapana. Lakini kwa kawaida yaanzia huko, yanapita kwenye kikao chenu cha RCC, baadaye yanakuja huku kwa ajili ya kuona kama kuna vigezo vimezingatiwa au hapana.

Sasa vigezo kwa upande wa Wilaya ni vingi kidogo lakini mambo makubwa hasa huwa kwanza, ni ukubwa wa eneo, eneo ambalo tunadhani Mkuu wa Wilaya anaweza akaliongoza bila matatizo makubwa sana ni kilomita za mraba zisizozidi 5000.

Lakini ni idadi ya watu, Mkuu wa Wilaya ili aweze kutimiza wajibu wake vizuri ni vizuri idadi ya watu ikawa kati ya 200,000 – 250,000 katika eneo ambalo analiongoza, inaweza ikawa chini kidogo au kuzidi kidogo lakini iwe katika eneo hilo la wingi wa watu.

Kwa hiyo, kama eneo lako unataka ligawiwe mara mbili tutakachoangalia kwanza ni ukubwa lakini tutaangalia je tukiligawa mara mbili upande mmoja utakuwa na idadi ya watu wangapi na upande mwingine utakuwa na watu wangapi.

Lakini formula hiyo siyo kwamba ikishasemwa basi muda wote inafuatwa, hapana! sehemu nyingine tunakuwa kidogo flexible au tunakuwa laini kidogo kwa kuzingatia pengine hali ya jiografia ya eneo lilivyo maana maeneo mengine ni visiwa, maeneo mengine yanaweza yakawa na utata mkubwa sana kama milima na kadhalika, wakati mwingine Serikali inakubali jambo hili kutokana na uhalisia wa eneo lenyewe lilivyo.
Kwa hiyo, kwa kweli Mheshimiwa Castor Ligallama ni kwa sababu sina uhakika na maombi yenu kama yaliletwa au hapana, lakini tunaweza tukaangalia na Mheshimiwa Celina Kombani tuone kama yaliletwa tukueleze kwa nini yalikataliwa.
  Records 1 to 3 of 6
 
Next Last
WHO IS WHO
Hon.Mongella, Ambassador Getrude Ibengwe
bunge
Ukerewe Constituency
Questions(0)
Supplementary Questions(22)
Contributions(58)
More Members »


POLIS DATABASE
polis
BUDGET 2010/11
Estimate of Public Expenditure Development votes and supply vote
SEARCH FOR MP
Region
Constituent
 
VIDEO /AUDIO CLIP
More Videos
PHOTO GALLERY
President Kikwete escorted by the Speaker of the National Assembly Hon. Sitta when arrived at Bunge ground in Dodoma on 21.8.2008.
More photos
CALENDAR OF EVENTS
 <<  < Sep 2010 >   >>
SMTWThFS
1234
567
8
91011
12131415161718
19202122232425
2627282930

More events

Copyright © 2003-2008 Tanzania Parliament. All rights reserved.
Designed and published by DataVision International (T) Ltd
Terms of Use | Disclaimer