ASK THE SPEAKER
GIF

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER
QUOTES FROM THE SPEAKER
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. "
5th March 2009 - Dar es Salaam.
INVITATION FOR TENDERS
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more
RESOURCES LINKS

Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project

WEBMAIL LOGIN


NEWSLETTER
Subscribe to our e-newsletter and be the first to know about new activities, events and resources.
Your email
GLOSSARY
By-elections
A by-election occurs when a seat in the National Assembly becomes vacant during the lifetime of a Parliament (i.e. between general elections).
Act
is a Bill approved by the House and formally agreed to by the President Assent. Once implemented, an Act is law and applies to country. Act of Parliament creates a new law or changes an existing law.
Read more
VISITORS TO THIS SITE
There have been 30501287 visitors to this websiteThere have been 30501287 visitors to this websiteThere have been 30501287 visitors to this websiteThere have been 30501287 visitors to this websiteThere have been 30501287 visitors to this websiteThere have been 30501287 visitors to this websiteThere have been 30501287 visitors to this websiteThere have been 30501287 visitors to this website
User online : 12
Home »Principal questions
Principal question
  email E-mail this to a friend email Printable version
Honourable Hafidh Ali Tahir  [CCM]
Dimani Constituency
Session No Principal Question No To the Ministry of Sector Date Asked
14 11 ENERGY AND MINERALS Energy 27 January 2009
Kwa kuwa hivi sasa Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara zimo katika mchakato wa kutafuta mafuta nchini kwa manufaa ya baadaye na kwamba hivi karibuni TPDC ilisema kuwa Zanzibar hakuna mafuta:-

(a) Je, ni sheria gani mojawapo inayoipa TPDC mamlaka ya kutoa kibali cha kutafuta mafuta Tanzania Zanzibar wakati wao siyo chombo cha Muungano?

(b) Je, mamlaka gani iliyowapa TPDC nguvu ya kutangaza kuwa Tanzania Zanzibar hakuna mafuta wakati Wazanzibari wanasema mafuta yapo?

(c) Je, kama TPDC si chombo cha Muungano Serikali haioni kuwa, kuitangazia Tanzania Zanzibar mambo yasiyo ya Muungano ni kuingilia mamb o yasiyoihusu?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #11 SESSION # 14
Answer From Hon. Malima, Adam Kighoma Ali
ENERGY AND MINERALS
NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI:

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hafidh Ali Tahir, Mbunge wa Dimani, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, TPDC iliundwa kwa tamko la Rais chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1969 Public Cooperations Act na kupewa majukumu ya kutafuta, kuzalisha na kuendeleza mafuta ya petrol chini ya Sheria ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta ya mwaka 1980 iliyopitishwa na Bunge hili Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Sheria hii ya utafutaji mafuta inampa Waziri wa Serikali ya Muungano mwenye dhamana ya petrol madaraka ya kufanya mazungumzo na wawekezaji na kuingia mikataba ya utafutaji na uzalishaji kwa niaba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Sheria ya utafutaji mafuta kifungu namba 17. Waziri ndiye anayetoa na kusaini leseni za utafutaji mafuta na siyo TPDC.

(b) Kuwepo ama kuwepo kwa mafuta katika eneo lolote lile kunaweza kuthibitishwa kwa uchambuzi wa taarifa za kitaalamu ambazo zinatokana na uchimbaji wa visima vya utafiti katika eneo husika. Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa pamoja ziliteua mshauri mwelekezi kuangalia pamoja na mengineyo ni jinsi gani Serikali mbili hizo zinaweza kuendeleza utafutaji wa mafuta katika maeneo ya Zanzibar na Pemba ambapo utafutaji unasuasua.

Pamoja na hayo, mshauri alipewa kazi kuchambua taarifa zilizopo na kutoa mawazo yake kama utafiti inabidi uendelezwe maeneo hayo. Mshauri mwelekezi aliona kuwa kwa taarifa ya kihistoria alizoonyeshwa mafuta yalikuwa hayajapatikana, yumkini alipendekeza ukusanyaji wa takwimu zaidi ufanyike ili tathmini nzuri iweze kufanywa. Ushauri huu aliutoa kwenye warsha ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Mheshimiwa Spika, kwa ujumla uwepo wa miamba tabaka Sedimentary Rocks ambayo kitaalamu duniani inafahamika kuwa na uwezekano wa kuandamana na mafuta Tanzania Bara na Visiwani zinaashiria uwezekano wa kuwepo kwa mafuta na gesi asilia na kwa maana hiyo uwekezaji zaidi unaweza ukaleta matokeo ya kina na ya uhakika zaidi kuhusu uwepo wa Nishati hizi.

(c)Mheshimiwa Spika, TPDC hawakutangaza kuwa Zanzibar hakuna mafuta. Katika warsha mbalimbali na taarifa wanazotoa TPDC kama ilivyo kwa maeneo mengine ya Jamhuri ya Muungano wanatoa taarifa ambazo ni matokeo ya tafiti zilizokwishawahi kufanywa na uwekezaji tofauti kwa upande wa tafiti zilizofanywa upande wa Tanzania Visiwani.

Tafiti hizo zimebaini ishara za uwepo wa mafuta yaani Indications au traces lakini kitaalam hiyo peke yake siyo ishara ya uwepo wa mafuta.

Hatua ya uwepo wa mafuta au gesi asilia inatambulika kitaalamu kama discovery. Hatua hiyo haijafikiwa na tafiti yoyote iliyowahi kufanywa Tanzania Visiwani.

Kama taasisi maalum kwenye nyanja ya mafuta ya petrol TPDC wana jukumu la kutoa ushauri wa kitalaamu na Serikali ina jukumu la kufanya maamuzi yanayostahili.

Kwa maana hiyo, kama chombo cha kitaifa cha kitaalam na cha ushauri, TPDC wana dhamana ya kutoa maoni yao ya kitaalamu yenye lengo na dhumuni la kujenga ili mradi maoni hayo yawe na makusudi ya kuboresha na kuendeleza juhudi za Serikali zote za Tanzania za kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii wananchi wa Taifa letu yanayotokana na uchumi wetu wenyewe na raslimali zetu wenyewe ikiwemo Sekta ya mafuta na gesi asilia. Kufanya hivyo kutakuwa siyo kuingilia mambo yasiyowahusu.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu ya mahitaji makubwa ya uwekezaji na teknolojia zinazohitajika kwenye masuala ya tafiti za mafuta na gesi asilia Wizara yetu inahimiza ushirikiano wa taasisi husika zote za Kiserikali na za Kibinafsi ikiwemo TPDC kuendeleza jitihada za makusudi kwa lengo la kuongeza na kuhamasisha uwekezaji katika sekta hii ambayo inaweza ikafungua milango mingi ya kujikomboa kiuchumi.

Records 1 to 1 of 25
 
Next Last
WHO IS WHO
Hon.Lwanji, John Paul
bunge
Manyoni Magharibi Constituency
Questions(30)
Supplementary Questions(30)
Contributions(109)
More Members »


POLIS DATABASE
polis
BUDGET 2010/11
Estimate of Public Expenditure Development votes and supply vote
SEARCH FOR MP
Region
Constituent
 
VIDEO /AUDIO CLIP
More Videos
PHOTO GALLERY
President Jakaya Kikwete posing in group photo on 21.8.2008. Seated from left is the PM, Hon.Pinda, Vice President Dr. Shein and his right hand side is the Speaker of the National Assembly, Hon. Sita and the Deputy Speaker Hon. Makinda. Standing from right is Hon. Hamad Rashid (Opposition leader), The acting Clerk of the National Assembly, Dr. Kashililah, Hon. Ndugai, Hon. Mhagama and Hon. Zubeir Maulid (bunge Charpersons)
More photos
CALENDAR OF EVENTS
 <<  < Sep 2010 >   >>
SMTWThFS
1234
567
8
91011
12131415161718
19202122232425
2627282930

More events

Copyright © 2003-2008 Tanzania Parliament. All rights reserved.
Designed and published by DataVision International (T) Ltd
Terms of Use | Disclaimer