|
|
| Home »Principal questions |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Honourable Stanley Jilaoneka Yono Kevela [CCM]
Njombe Magharibi Constituency |
|
| 5 |
109 |
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT |
Transport/Road |
10 November 2006 |
Kwa kuwa Madaraja ya Ilembula ¿ Matowo na Daraja la Korintho - Ilembula yaliahidiwa kujengwa na kukarabatiwa mapema na Serikali pamoja na kukarabati barabara zinazounganisha vijiji hivi ambavyo ni kero kubwa:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha madaraja hayo na barabara hizo?
|
| ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #109 SESSION # 5 |
 |
Answer From Hon. Kombani, Celina Ompeshi
REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT |
|
NAIBU WAZIRI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Yono Stanley Kevela, Mbunge wa Njombe Magharibi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa ujenzi wa madaraja kwenye barabara za Ilembula- Korintho na Ilembula ¿ Matowo pamoja na kukarabati barabara hizi ni mojawapo ya hatua kubwa ya kuwapunguzia kero wananchi wa Jimbo la Njombe Magharibi na Wilaya ya Njombe kwa ujumla.
Ujenzi wa daraja kwenye Mto Halali unaokatiza kwenye barabara ya Ilembula hadi Korintho ulikamilika rasmi mnamo mwezi wa Oktoba 2005 na uligharimu jumla ya shilingi 35.5 milioni na ujenzi wa daraja kwenye mto huo huo wa Halali unapokatiza kwenye barabara ya Ilembula hadi Matowo unaendelea na unategemewa kukamilika ifikapo mwezi Desemba 2006 kwa gharama ya shilingi 20.64 milioni. Aidha, barabara ya Palangawamu hadi Ilembula (km.12), ambayo inaunganisha Vijiji vya Palangawamu, Matowo na Ilembula ilifanyiwa matengenezo mnamo mwaka 2004 na hali yake siyo mbaya isipokuwa ujenzi wa daraja la Halali ambao unaendelea kwa sasa.
Mheshimiwa Spika, Serikali ikishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe inaendelea na ukarabati wa barabara ya Ilembula hadi Luduga yenye (km.9) kwa gharama ya shilingi 26.3 milioni na ukarabati unategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Novemba 2006.
|
|
Records 1 to 1 of 23 |
|
|
|
|
|