|
|

Hon.Samuel Sitta(MP)
Online interactive forum with the SPEAKER |
|
" One of the core duties of the Legislature is to oversee the functions of the Government in power and advise it appropriately whenever any pertinent issue of national interest arises. " |
| 5th March 2009 - Dar es Salaam. |
|
|
 |
Tender for the Financial year 2010/2011
Read more |
|
Parliamentary Resources
National Website
Prime Minister's Office website
National Electoral Commission website
Africa4All project
|
|

|
|
|
|
| General election |
In a general election the adult population of the TANZANIA chooses a candidate to represent each constituency in the House. Every MP has to stand for re-election. They are usually held every five years. |
| Parliamentary Committees |
The services of the Speaker and his deputies, and those of the permanent officers who are at the Speaker's disposal are not the only auxiliaries to which the House has recourse for the dispatch of its work: with a view to the efficient performance of its role it is accustomed to Parliament to appoint temporary composite bodies from among its own membership, which we refer to as Committees. |
Read more
|
|
|
|
|
| Home »Answers |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Honourable Dr. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya [CCM]
Kwela Constituency |
|
| 2 |
3 |
INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT |
Works |
7 February 2006 |
Kwa kuwa upo umuhimu wa kibiashara kati ya Tanzania na Zambia, Kongo (DRC) na Burundi;
Je, Serikali inaweza kutamka rasmi ni lini Bandari ya Kasanga itakamilika kujengwa na lini barabara ya lami kati ya Sumbawanga na Mbale Zambia itajengwa?
|
| ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #3 SESSION # 2 |
 |
Answer From Hon. Mahanga, Dr. Milton Makongoro
INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT |
NAIBU WAZIRI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Miundombinu kabla sijajibu swali la Mheshimiwa Dr. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, Mbunge wa Kwela, napenda kutoa maelezo ya utangulizi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kibiashara uliopo kati ya Tanzania na nchi za jirani za Zambia, Kongo (DRC) na Burundi. Kwa kuzingatia umuhimu huo, mwezi Novemba, 2004 Serikali ya Awamu ya Tatu ilianzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari zote nchini Tanzania Ports Authority (TPA) kwa madhumuni ya kusimamia na kuziendesha Bandari za Maziwa kwa kasi kubwa zaidi. Aidha, ipo mipango na mikakati ya kutumia kikamilifu fursa ya kuwa na bandari hizi ili ichangie vema katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo mafupi, sasa napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dr. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2005/2006, Serikali ilitenga kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya kuziendeleza Bandari za Maziwa. Kati ya hizo, Bandari za Ziwa Tanganyika ikiwemo Kasanga zimetengewa shilingi milioni 150. Kiasi hiki cha fedha zilizotengwa ni kidogo sana ikilinganishwa na hali mbaya ya miundombinu katika bandari za Maziwa. Juhudi za kutafuta fedha zaidi zinaendelea ambapo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika mwaka wa fedha wa 2005/2006, imepangwa kufanya utafiti kamambe na tayari Benki ya Dunia imekubali kutoa Dola za Kimarekani 800,000 kwa kazi hiyo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara, Serikali inatekeleza miradi ya ujenzi wa barabara kuu za lami kwa kufuata Kanda Kuu za Usafirishaji ambayo nayo inategemea upatikanaji wa fedha. Kwa msingi huo miradi hii ya barabara kuu za lami inatekelezwa kwa awamu. Kwa upande wa Ukanda wa Usafirishaji wa Magharibi ambao unajumuisha barabara ya Sumbawanga - Kasesya - Mbala kule Zambia, Serikali imeona ianze kwanza ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara ya Tunduma kwenda Sumbawanga na hatimaye Sumbawanga - Mpanda - Kigoma kwa awamu. Pia ujenzi wa sehemu ya barabara ya Sumbawanga - Kasesya - Mbale kwa kiwango cha lami utatekelezwa kwa awamu itakayofuata kutegemea upatikanaji wa fedha. Kutokana na umuhimu wa barabara hiyo, matengenezo kwa kiwango cha changarawe yataendelea ili kuhakikisha kuwa barabara wakati wote.
|
|
|
Records 1 to 1 of 181 |
|
|
|
|
|