|
|
| Home »Contribution |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Tahir, Hafidh Ali[CCM]
Dimani Constituency |
|
|
|
|
|
| 16 |
29 |
15 July 2009 |
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2009/2010 Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo |
Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba Mheshimiwa Waziri anisaidie maelezo yafuatayo. Nilipokuwa nachangia leo sikuchangia kuhusu TFF na ZFF sikugusa kabisa. ZFA kama Zanzibar katika sakata ambalo linaendelea hivi sasa tarehe 21 litakuwa limekwisha. Tumekwishasafiri sana sisi. Nilichochangia kwa maandishi leo na kwa kusema ni Utaifa wa Tanzania ndani ya Bunge na hili namwomba sana Mheshimiwa Waziri akalifanyie kazi kama nilivyosema baina yake yeye na Waziri wa Michezo Zanzibar. Sisi tunakufa, watabaki vijana wetu waje kurithi mambo mazuri. Nilichochangia leo ni kumwomba Mheshimiwa Waziri akae na mwenzie atoe agizo au maelekezo kwamba uwakilishi wa Tanzania nje unaweza ukasajiliwa na Tanzania Bara kama ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu wao ndiyo wenye mambo ya nje.
Lakini vyama vinapojisajili huko nje wakishapata usajili humu ndani warudi waweke taratibu na vyama vingine vya Zanzibar ili wanapokwenda nje ijulikane kama ni Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ndicho nilichosema. Sasa namwomba Mheshimiwa Waziri akubaliane na mimi kwamba ili Tanzania itambulike huko nje, vyama vyetu humu ndani viwe na Katiba ambayo inazungumzia kwamba ndani ya Jamhuri ya Muungano tuna vyama viwili lakini tukienda nje tuna Utanzania ambao tunakwenda nao. Sikuzungumzia ZFA hapa. Sasa namwomba Mheshimiwa Waziri ili kuliweka Taifa letu vizuri na vizazi vije kurithi mambo mazuri hili lifanyike tuondoe hii mizozo.
|
|
Records 1 to 1 of 34 |
|
|
|
|
|