|
|
| Home »Contribution |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Kevela, Stanley Jilaoneka Yono[CCM]
Njombe Magharibi Constituency |
|
|
|
|
|
| 20 |
15 |
24 June 2010 |
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2010/2011 - Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi |
Mheshimiwa Naibu Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dr. John Pombe Magufuli kwa hotuba yake nzuri na endelevu. Pia nampongeza sana Mhe. Dr. Wanyancha kwa jinsi alivyo mchapa kazi akisaidiana na Waziri wake pamoja na Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara.
Mheshimiwa Naibu Spika, hoja ninayochangia ni juu ya ufufuaji wa Viwanda vya Ngozi, Kiwanda cha Nozi cha Moshi kilichobinafsishwa bado matumizi yake ni kidogo sana. Natoa ushauri kuwa Kiwanda hicho kingeboreshwa sana ikiwezekana kipelekwe kwenye maeneo ya mifugo kama vile Mwanza, Shinyanga, Rukwa, Iringa au Dodoma.
Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru na kupongeza sana kwa Wizara yako kwa kutupatia majosho na malambo kwenye Jimbo la Njombe Magharibi. Majosho hayo ni Kanamalenga, Mpululu, Visuka, Mambegu na Saji.
Mheshimiwa Naibu Spika, vile vile machinjio ya kisasa ya Ilembula nayo nakupongeza sana. Ombi, tunaomba gari la kubebea nyama kutoka machinjio hayo ya kisasa hadi Kwamalaji pale Ilembula mjini machinjio yako umbali wa kilomita tatu hivi. Pia machinjio hayo hakuna maji na umeme.
Umoja wa Wenyebucha wanaomba wawekewe umeme, maji na gari la kisasa ili kulinda usalama wa walaji, mpaka sasa vifaa vinavyotumika ni mikokoteni michakavu na haina ubora kabisa. Tunaomba Wizara yako ishirikiane na Halmashauri ya Njombe sasa Halmashauri ya Wanging’ombe, Umoja huo uko Ilembula.
Mheshimiwa Naibu Spika, pongezi zingine kwa kiwanda cha machinjio cha Ruvu kuanzishwa kitasaidia sana wafugaji kupata mapato mazuri kwa Serikali na wafugaji.
Mwisho, nashauri vyuo vya Mifugo na Semina mbalimbali zitiliwe mkazo wa kutosha. Tukiwa na wataalam wengi wafugaji watafuga kwa faida na kuongeza pato la Taifa.
|
|
Records 1 to 1 of 62 |
|
|
|
|
|