|
|
| Home »Contribution |
|
| |
 |
E-mail this to a friend |
 |
Printable version |
 |
Karamagi, Nazir Mustafa[CCM]
Bukoba Vijijini Constituency |
|
|
|
|
|
| 20 |
19 |
29 June 2010 |
Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2010/2011 – Wizara ya Miundombinu |
Mheshimiwa Spika, mchango wangu ni mdogo ukijikita kwenye maeneo machache. Kwanza niipongeze Serikali kupitia kwa Wizara ya Miundombinu kwa kazi kubwa sana iliyofanyika ya kufungua nchi haswa kwa upande wa barabara, lakini mwanga unaonekana.
Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziri anisaidie kufafanua mikakati iliyopo juu ya uendelezaji wa uwanja wa ndege wa Bukoba kwa kutuhakikishia kuwa kuna mpango wa kuweka lami ili utumike wakati wote wa kiangazi na masika, kivuko cha kuunganisha Bukoba na Uganda kilichowekwa kijiji cha Rubafu katai ya Rubafu – Bukoba vijijini. Mradi huu chini ya Afrika Mashariki unasemekana umeanza kupungukiwa fedha. Tunapenda kuhakikishiwa kuwa mradi huu utakamilika. Pia kivuko cha Kyenyabasa kinachounganisha kati ya Bujugo na kata ya Kasharu kilichofungua injini ambayo wakati wote inaharibika haribika na kulazimika kuvutwa kwa mkono, je, lini tatizo hili litamalizika?
|
|
Records 1 to 1 of 42 |
|
|
|
|
|